kilimo bora cha nyanya
KILIMO BORA CHA NYANYA
zao la nyanya shambani |
AINA
Ziko nyingi kama fupi kiasi (Semi Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAAA; Semi-determinent
1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-
B; Aina Ndefu (Indeterminent)
-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU
AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVAC; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima
MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigradeUDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo. NAFASI YA KUPANDA
-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapanda double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA
Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)
Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)
Upandaji maarufu ni sm 60×60 mche mpaka mche na mstari mpaka mstari
KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 25-30 kwa hybrid (F1 ama mbegu10667) . .UPANDAJI AMA KUSIA
Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowote utakao, na kisha chora vimifereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu.Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)
MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.
ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA SIKU 21-25 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.
MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI
Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung’oa miche, na shamba pia liwe limemwagiwa vya kutosha.-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate weka DAP 5 gm na changanya ile mbolea kwenye shimo na udongo ili mizizi ya mche isigusane na mbolea kwa sababu inaweza kusababisha kuungua na madhara mengne.
Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo baada ya kupandikiza hakikisha unamwagia maji vzur kwa mimea uliyopanda
BAADA YA KUPANDIKIZA
Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majaniDawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao
Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipigwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana saa 6 hadi saa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shapeless
MATUNDA YAKIJA
Ni muhimu kuzungusha chini katika mizizi mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking
WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)Magonjwa
Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)
MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 90 HADI 120 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA KUTOKANA NA HALI YA HEWA YA ENEO HUSIKAMAVUNO
Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 35SOKO
Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanamuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..
WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA
DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inaweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yule mother kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana
Kwa utaalam Na mbegu kwa kilimo hiki tuchek kwa +255757808824 ama saringo50@gmail.com
KARBU NORTAN
Leave a Comment