MTAMBUE MDUDU MTU (APEFLY)
MTAMBUE MDUDU MTU
Spalgis epius epius( jina la kitaalamu)
Himaya:Mududu
Familia: Lycaenidae
Jenasi : Spalgis
Spishi: epius
Jina linalojulikana: Apefly
Urefu wa mabawa: 10-14
mm
Historia yake ya maisha: Bado haijakamilika
Apefly ni mdudu ambaye amekuwa gumzo kwenye mitandao mingi ya kijamii, akibatizwa kwa jina la MDUDU MTU.
Ubatizo wa hili jina umetokana na muonekano wake kufanana kwa karibu na sura ya binadamu ama Tumbili.
HATUA ZA UKUAJI WA APEFLY KATIKA PICHA
Taarifa zimeenea kuwa huyu mdudu anapatikana kwenye mboga za majani.
KwaTaarifa zaidi tembelea mtandao wa RESEARCHGATE.NET unaelezea matokeo toka maabara kuhusiana na chakula cha apefly na kiwango cha ulaji wake kutokana na kila hatua yake ya ukuaji.
Kitu ambacho jamii inatakiwa kujua ni kwamba kati ya wadudu ambao wanafaida kwa mkulima anaesumbuliwa hasa na wadudu spishi ya MEALYBUG (Kidukari sufu) ,APEFLY ni mdudu ambaye anajipatia chakula kupitia huyu mdudu.
Picha ikimuonyesha Apefly akiwa kwenye papai ambalo limeshambuliwa na Mealybug ( Kidukari Sufu) |
Ukikutana na apefly kwenye mimea yako basi haina haja ya kutumia kemikari kwa sababu zile kemikari zinaweza leta madhara kwa hawa wadudu wenye faida kwenye mazao yetu.
Na kama utatumia basi utaua tatzo na suluhisho pamoja.
Njia ya kujikinga na mealybug ama Kidukari sufu ni
Mealybug jinsia ya kike akiwa chini ya jani la pasheni |
- Usizidishe maji na mbolea-Vidukari sufu huvutiwa na mmea wenye kiwango kikubwa cha mbolea ya Naitrojeni na ukuaji laini.
- watoe kwa mkono na punguza majani yaliyoshambuliwa zaidi
- Imarisha ubora wa udongo wako kwa kuufanya kuwa na virutubisho vya kutosha kwa sababu mmea ambao umepata virutubisho vya kutosha unaweza himili uvamizi wa hawa wadudu.
- Tumia maji yenye presha kubwa kuwaondoa hawa wadudu katika majani na hakikisha pale chini hakuna siafu ama sisimizi kwa sababu watarudishwa juu ya mmea tena.
- Tumia mwarobaini pia inasaidia
- ama kikemikari tumia Sumu zenye kiwatilifu cha
chlorpyriphos 25 EC na kiwango ni 2ml kwa lita ama profenophos 50 EC @ 2 ml au thiodicarb 75 WP 2 Gram kwa lita.
IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA; Norbelt poncian (mmiliki wa blog ya www.nortantz.blogspot.com)
TEMBELEA NA KWA SHIDA YA ELIMU NA UJUZI JUU YA MALI MBICHI TUTAFTE KWA:
+255757808824
AU
SARINGO50@GMAIL.COM
Leave a Comment