JINSI YA KUPIKA BIRYANI YA MBOGAMBOGA
Biryani ya mbogamboga
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani
la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki
kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.
Mahitaji:
½ kg mchele wa basmatiKitunguu maji kikubwa 1
Nyanya 1 kubwa
Karoti 1 kubwa
Njegere robo kikombe
Kiazi ulaya 1 kikubwa
Tangawizi za kusaga kijiko 1
Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1
Karafuu kijiko 1
Majani ya kotimili fungu 1
Maziwa ya mtingi ¼ kikombe
Chumvi na pilipili kiasi
Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani
Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani
Mafua ¼ lita
Maandalizi:
Chemsha mchele na kisha weka pembeniOsha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya
Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa
ENDELEA KUTUTEMBELEA NASI TWA KUKARIBISHA
Leave a Comment