KILIMO BORA CHA MCHICHA KIBIASHARA

                            KILIMO CHA MCHICHA

UTANGULIZI

   Mchicha ni moja kati ya  mazao rahisi sana kulimwa na haina masharti mengi  wakati wa kulima had kuvunwa.
mchicha huliwa na binadamu pamaoja na wanyama na pia ina vitamin A na C ndani yake, hutumika kama mboga inaweza kuchemshwa na unaweza kutumia mchuzi wake kama supu. pia kuku wanaweza kupewa na kudonoa majani yake.
Na pia mchicha hustawi katika aina yoyote ya udongo na hali ya hewa yoyote

KUANDAA SHAMBA.

   Ili kuandaa shamba kwaajili ya kupanda mchicha inatakiwa shamba lipaliliwe vizuri na magugu yote kuondolewa shambani
na pia shamba linatakiwa kuandaliwa mwezi mmoja  kabla ya kupanda mbegu za mchicha.

KUANDAA KITALU

   Kitalu ni muhimu sana kwa kilimo cha mchicha
kinatakiwa kiwe na upana wa mita1 yaaani 100 sentimita na kinatakiwa kiinuke juu na kiwe na kingo ili kusaidia kuweka unyevunyevu ndani ya kitalu
pia kinatakiwa kutifuliwa vizuri ili kusaidia maji na hewa kupenya ndani ya kitalu
napia unatakiwa kuweka mbolea ya samadi kabla na kukimwagulizia kitalu angalau wiki moja kabla ya kupanda asubuhi na jion.
pia unashauriwa kupanda ntama au mahindi kuzunguka shamba ili kusaidia wadudu na ndege waalibifu kutoingia ndani ya shamba.

 KUPANDA MBEGU

Kuna njia mbili za kupanda mbegu ya mchichi
 1. kusambaza- yan mbegu zinasambazwa ndani ya kitalu bila kua  na m pangilio
 2. kupanda kwa msital- hii ndo njia nzuri na ambayo nitaielezea kwa upana kidogo
hapa unatengeneza mistari ndani ya kitalu ambayo utamwaga mbegu ndani ya hii mistari na nafasi kati ya mstali kwa mstali ni 10 had 15 cm.
Bwana Valerian akisia mbegu zake za mchicha katika kitalu kilichopitwa kwa kuchanganya mchanga na mbegu zake za mchicha.


kabla ya kupanda mbegu unatakiwa kuhakikisha mbegu zimechanganywa na mchangam wenye saizi sawa na mbegu zako za mchicha ili kuepusha mbegu kupepeluka na kupunguza upotevu mwingi wa mbegu.na hii njia husaidia kwa mbegu aina nyingi hasa unaposia kitaluni.
unaweza kuweka vikombe viwili vya mchanga katika kila kikombe kimoja cha mbegu
na  pia unatakiwa kumwagilizia kitalu kabla ya kupanda.


MUHIMU

Unatakiwa kumwagilizia mchicha kila sku asubuhi na jion lakn usimwagilize majimeng kupita kipimo na wala usimwagilizie maji machache
pia unatakiwa kupalilia unapoona magugu yamekua mengi kwenye kitalu

  KUVUNA

mchicha ukipewa huduma nzuri unavuna ndani ya wiki 3
na pia unaweza kuvuna kwa kung'oa au kwa kukata


Kwa ushauri na utaalamu tutafte kwa namba +255757808824 ama saringo50@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.