UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION

UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION


 

UTANGULIZI

Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash ama Zucchin. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.

HALI YA HEWA

Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua : kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.

Hali ya Udongo

Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio mchanganyiko wa mchanga na udongo tifutifu na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.

Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.

Kitaluni

Kwa ulaini wa mizizi ya mimea jamii ya matikiti sishauri mkulima KUSIA mbegu(sowing) kwa kutumia vitalu vya chini,Bali tumia vitalu vya trei(tray)
Ila kama imeshindikana basi ni bora ukapanda direct shambani 
Kama utatumia trei kama vitalu basi siku za kusia mpka kuhamishia shambani ni siku 12-15 tu.
Tumia mbegu moja kila shimo.
sowing trays
Trei zinazotumika kama njia mbadala ya  kusia miche ya aina nyingi nyingi za mbegu za mboga mboga badala ya kutumia vitalu vya chini ama (ground nurseries)
mizizi ya matikiti maji
Mwonekano wa nje wa miche ya tikiti iliyopandiwa kwenye vitalu vya trei ikiwa na mizizi yake yote .


UANDAAJI WA SHAMBA

Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa.

UPANDAJI

Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 2-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2  moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu cha chini (Ground Nursery) kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 50 au 60 kutoka shina hadi shina na upana wa tuta ni mita 1 ila upana wa tuta moja mpaka lingne ni mita 2 kutoka mstari hadi mstar. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Pia vzur kupanda mbegu zaidi ya 2 kwenye shimo kwa sababu asilimia nyingi za mbegu chota ni 85-100 hvyo ukitumia mbegu zaidi ya moja ni kujiongezea garama zisizo za mhimu.

UPUNGUZAJI WA MIMEA

  katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.

MATANDAZO (MULCHES )

Matandazo ina maana ya kutumia plastic mulching ama nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
Mtambazo ya nyasi zilizo kauka kwenye tuta katika miche wa tikiti maji

Matambazo ya plastic (plastic mulching)



UWEKAJI WA MBOLEA

 

STAGE YA MMEA
AINA YA MBOLEA
KIWANGO CHA KUTUMIA MBOLEA
NJIA YA KUWEKA MBOLEA KATIKA MCHE
Kitaluni
Calcium Nitrate (CAN)
2.5 GRAMS/LITA
KUDIRENCHI(mbolea kuchanganya na maji kisha kumwagilia ule mchanganyiko kwenye shinda la mche)
20+20+20+ME
2.0 GRAMS/LITA
KUDIRENCHI
SIKU YA KUHAMISHIA SHAMBANI
DIAMMONIUM SULPHATE
(DAP)
5gm/shimo
KUWEKA PUNJE SEHEMU AMBAYO UTAHAMISHIA MCHE
Calcium Nitrate (CAN)
60gm/lita 16 za maji
KUDIRENCHI
UKUAJI WA MAJANI
UREA +MOP(MURIATE OF POTASH) 1:1  baada ya siku 21 baada ya kuhamishia miche shambani
10gm/kila mmea
Kuweka mchanganyiko wa mbolea hizi mbili sentimeta 5  pembeni ya mche
Kuweka mchanganyiko wa mbolea hizi mbili sentimeta 5  pembeni ya mche
15gm/mmea
Weka punje za mbolea kwenye shimo Sentimeta 5 pembeni ya mche
UKUAJI WA MAUA NA MATUNDA
UREA +MOP(MURIATE OF POTASH (1:2)
10gm/mmea
Kuweka mchanganyiko wa mbolea hizi mbili sentimeta 5  pembeni ya mche
Baada ya siku 7 weka tena UREA +MOP(1:3)
20gm/mmea
Kuweka mchanganyiko wa mbolea hizi mbili sentimeta 5  pembeni ya mche
Baada ya siku 7 weka NPK 14+14+14
15gm/mmea
Weka punje za mbolea kwenye shimo Sentimeta 5 pembeni ya mche
UREA +MOP(1:2)

Weka punje za mbolea kwenye shimo Sentimeta 5 pembeni ya mche

.

UMWAGILIAJI

Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.

MAUA NA MATUNDA

Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii hufanywa kwa , kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

MAGONJWA NA WADUDU

Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea.
Document inayofuata nitaelezea magonjwa na wadudu kwenye hili zao


UVUNAJI MATIKITIKI

abla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea
Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Soko la matikiti maji
Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka 3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.
Mavuno
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya
TANI 15-36 kwa hekta moja.

  KWA MAHITAJI YAKO YA MBEGU HIZI ZA KISASA  NA UTAALAMU WASILIANA NAMI KWA NAMBA HIZO CHINI.KWA WA MIKOANI

+255757808824


No comments

Powered by Blogger.